Pata matokeo ya kidato cha sita kwa kuclick link hiihttp://www.necta.go.tz/results2016/ACSEE2016/index.htm
SLOBNEWS
Friday, 15 July 2016
Saturday, 21 May 2016
Majina Ya Kidato Cha Sita 2016 Waliochaguliwa na JKT kwa mafunzo
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2016, kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria.
Sanjari na uchaguzi huo, JKT limewapangia makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 01 - 05 Juni 2016.
Sanjari na uchaguzi huo, JKT limewapangia makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 01 - 05 Juni 2016.
BOFYA HAPA KUPATA ORODHA KAMILI
Kambi ya KANEMBWA---KIGOMA
KAMBI YA RWANKOMA--MARA
KAMBI YA BULOMBORA--KIGOMA
KAMBI YA MSANGE--
Sunday, 15 May 2016
Balaa usafiri wa bure D’salaam
Hata hivyo, bure hiyo ni gharama. Baadhi ya abiria waliotumia usafiri wameshapoteza mali zao kwa vibaka, wameumia kutokana na kubanana huku kukiwa na kundi kubwa la wazururaji ambao husafiri na mabasi hayo bila kushuka popote.
Dar es Salaam. Haijapata kutokea kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, kusafirishwa bure, lakini imetokea kwa siku tano mfululizo baada ya kuanza mabasi yaendayo kasi (Udart).
Hata hivyo, bure hiyo ni gharama. Baadhi ya abiria waliotumia usafiri wameshapoteza mali zao kwa vibaka, wameumia kutokana na kubanana huku kukiwa na kundi kubwa la wazururaji ambao husafiri na mabasi hayo bila kushuka popote.
Mbali na bughudha kwa abiria, tayari mabasi hayo mapya yameshaanza kuharibiwa baadhi ya vifaa, kutokana na kukosekana ustaarabu kwa watumiaji. Huo ndiyo usafiri wa mabasi yaendayo haraka.
Saturday, 14 May 2016
Mahakama yaamuru maiti inayogombewa izikwe Kikristo
Mtoto huyo alifariki dunia Mei 5, mwaka huu katika kijiji cha Msingisi Wilaya ya Gairo, lakini ulitokea mvutano kati ya wazazi kuhusu dini ya kumzikia mtoto kwakuwa wazazi wana imani tofauti za dini, na kila mzazi alitaka kumzika kwa dini yake.
Morogoro. Mahakama ya Wilaya ya Morogoro imeamuru mwili wa mtoto, David Mng’ombe (8) mkazi wa Gairo kuzikwa kwa imani ya dini ya Kikristo baada ya kuwapo kwa mvutano baina ya baba wa mtoto, Shukuru Mng’ombe na mama yake, Emilia Chitemo kuhusu dini.
Mtoto huyo alifariki dunia Mei 5, mwaka huu katika kijiji cha Msingisi Wilaya ya Gairo, lakini ulitokea mvutano kati ya wazazi kuhusu dini ya kumzikia mtoto kwakuwa wazazi wana imani tofauti za dini, na kila mzazi alitaka kumzika kwa dini yake.
Tuesday, 10 May 2016
Rodrigo Duterte ashinda urais Ufilipino
Meya wa jimbo aliyeongoza kampeni kali ya urais Ufilipino, Rodrigo "Digong" Duterte ameshinda uchaguzi huo kufuatia kujitoa kwa wapinzani wake.
Licha ya kwamba matokeo rasmi hayajatangazwa, mpinani wake mkuu Mar Roxas amekiri kushindwa baada ya kura zinazohesabiwa kudhihirisha Duterte anaongoza kwa kura nyingi.
Duterte amesema anakubali jukumu hilo kwa "unyenyekevu mkubwa".
Mgombea huyo aliye na umri a miaka 71 alizusha mzozo wakati wa kampeni kwa matamshi yake makali.
Ametaja ufanisi kutokana na msimamo wake mkali kutii sheria na kuimarisha utulivu.
Rekodi yake kama Meya asiyekubali uhalifu wa mji wa kusini Davao, ambao kwa wakati mmoja ulitambulika kwa kukithiri uhalifu, ulichangia Duterte kusifiwa kuwa muadhibu na sifa hiyo ilisambaa miongoni mwa wapiga kura.
Mambo yaliogubika kampeni za uchaguzi ni kukithiri kwa rushwa pamoja na umaskini na ukosefu wa usawa miongoni mwa ria aUfilipino licha ya ukuwaji wa uchumi ulioidhinishwa na rais anayeondoka Benigno "Noynoy" Aquino.
Matamshi makali ya Duterte dhidi ya uhalifu -- hata kutishia kuwaua wahalifu -- yanaonekana kuungwa mkono na wapiga kura wengi -- lakini yameshutumiwa na makundi ya kutetea haki za kibinaadam
Sunday, 8 May 2016
Orodha ya Fifa: Tanzania yashika mkia Afrika Mashariki
Taifa la Tanzania limeorodheshwa la mwisho Afrika Mashariki katika orodha mpya ya shirikisho la soka duniani Fifa.
Tanzania imeorodheshwa katika nafasi 129 duniani huku ikishika mkia miongoni mwa mataifa ya Afrika Kusini.
Taifa linaloongoza katika eneo hili la Afrika ni Uganda ikiwa katika nafasi ya 72,Rwanda katika nafasi ya 87,Kenya katika nafasi ya 116 na Burundi katika nafasi ya 122.
Kwa jumla Argentina bado inaendelea kuongoza katika orodha hiyo ikifuatiwa na Ubelgiji na baadaye Chile katika nafasi ya tatu.
Mabingwa wa kombe la dunia Ujerumani wanashikilia nafasi ya 5 huku Uhispania na Brazil zikifuata katika nafasi ya tano na sita mtawalia.
Friday, 6 May 2016
Bomoabomoa yaanza Nairobi baada ya mkasa
Serikali ya jimbo la Nairobi imeanza kubomoa nyumba ambazo maafisa wanasema hazifai kuishi watu.
Shughuli hiyo inatekelezwa baada ya jumba moja la makazi la ghorofa sita kuporomoka Ijumaa wiki iliyopita na kuua watu 36.
Watu karibu 70 bado hawajulikani walipo.
Shughuli ya leo imelenga nyumba nane ambazo zimekuwa zikiishi watu karibu 600.
Baadhi wamekuwa wakijaribio kuokoa mali yao mapema leo.
Baadhi ya wakazi wamelalamika kwamba hawana kwa kwenda.
Subscribe to:
Posts (Atom)