Hata hivyo, bure hiyo ni gharama. Baadhi ya abiria waliotumia usafiri wameshapoteza mali zao kwa vibaka, wameumia kutokana na kubanana huku kukiwa na kundi kubwa la wazururaji ambao husafiri na mabasi hayo bila kushuka popote.
Dar es Salaam. Haijapata kutokea kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, kusafirishwa bure, lakini imetokea kwa siku tano mfululizo baada ya kuanza mabasi yaendayo kasi (Udart).
Hata hivyo, bure hiyo ni gharama. Baadhi ya abiria waliotumia usafiri wameshapoteza mali zao kwa vibaka, wameumia kutokana na kubanana huku kukiwa na kundi kubwa la wazururaji ambao husafiri na mabasi hayo bila kushuka popote.
Mbali na bughudha kwa abiria, tayari mabasi hayo mapya yameshaanza kuharibiwa baadhi ya vifaa, kutokana na kukosekana ustaarabu kwa watumiaji. Huo ndiyo usafiri wa mabasi yaendayo haraka.
No comments:
Post a Comment